Mtu mmoja anayesadikika ni mvulana wa miaka 17 mwenye asili ya Afghanistan amewashambulia abiria waliokuwa kwenye Treni Kusini mwa Ujerumani na kuwajeruhi watu wanne kabla ya kuuawa na Polisi.

Polisi mjini Wuerzburg wamesema kuwa abiria wanne wamejeruhiwa vibaya na wengine 14 wamepata msaada kutokana na mshtuko walioupata katika tukio hilo.

Polisi nchini humo wamesema kwamba hakuna taarifa yeyote kuhusu sababu ya kutekelezwa kwa shambulio hilo.

Lakini mpaka sasa hakuna ishara ama taarifa zozote kuwa shambulio hilo lilikua la kigaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *