Watu 4 wamepoteza maisha na wengine 22 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria aina ya Coaster linalofanya safari zake Mbeya na Chunya kupinduka katika Kijiji cha Majimazuri, Wilaya ya Mbeya Vijijini katika Barabara ya Mbeya/Chunya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari amesema kuwa ajali hiyo imetokea mnamo tarehe jana majira ya saa 9:50 Alasiri ikihusisha gari lenye namba za usajili T.841 BRW aina ya Isuzu basi likitokea Wilaya ya Chunya kwenda Mbeya.

Amesema gari hilo lililokuwa likiendeshwa likiendeshwa na dereva aitwaye ELIA ISACK [37] Mkazi wa Chunya liliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo kwa abiria wanne ambao ni HAWA MOHAMED [30] mkazi wa Chunya, Mtoto mdogo wa miaka 2 wa kiume ambaye bado kufahamika jina lake na wanaume wawili ambao hawakufahamika majina yao.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kwamba majeruhi wote wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na dereva amekamatwa huku upelelezi ukiwa bado unaendelea.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *