Watu wanne wajeruhiwa  baada ya gari moja lililokuwa kwenye msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kutoka Mtwara kwenda wilayani Tandahimba kuanguka maeneo ya Nanguruwe mkoani humo.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Ligula ambapo wanapatiwa huduma kwenye Hospitali hiyo.

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, Makamu wa rais yupo ziarani mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara.

Tovuti hii itakuletea taarifa juu ya chanzo cha ajali hiyo iliyotokea Mtwara pamoja na maendeleo ya majeruhi hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *