Watu wanne wamefukiwa na kifusi katika machimbo ya kokoto, Golani yaliyopo eneo la Pugu Jiji la Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa, tukio hilo lilitokea jana Alhamisi majira ya saa 8 mchana ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa vyombo vya uokoaji vimefanikiwa kupata watu wawili ambapo mmoja alikuwa tayari amekwishafariki dunia.

Mjema ameeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na mtu wa pili  aliyeokolewa akiwa hai alikuwa amevunjika mguu ambaye pia amepelekwa Muhimbili kwa ajili ya kutibiwa.

Mkuu wa wilaya huyo  ameeleza kuwa, wawili waliobakia hawajafanikiwa kuokolewa kutokana na changamoto ya mvua nyingi zinazoendelea kunyesha pamoja na ubovu wa miundombinu ya njia za kupitishia mitambo ya uokoaji.

Kwa upande Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salumu Hamduni amesema kuwa, wanachokisubili mpaka sasa ni mtambo maalumu kwa ajili ya ukoaji. Taratibu za kufukua miili ya watu iliyobaki ndani ya kifusi bado inaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *