Watu 4 wamefariki na 15 kujeruhiwa baada ya basi dogo kugonga lori katika Kijiji cha Lusanga Muheza mkoani Tanga.

Ajali hiyo mbaya imetokea katika Kijiji cha Lusanga wilayani Muheza ambapo basi aina ya Coaster likitokea Tanga kuelekea Korogwe kugonga lori kwa nyuma na kusababisha vifo hivyo.

Baada ya kuokolewa Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali Teule ya Muheza kwa ajili ya matibabu zaidi.

Ajali hiyo imetokea siku chache baada ya kutokea ajali ya wanafunzi 32 jijini Arusha siku ya jumamosi.

Wanafunzi hao wanaagwa leo katika uwanja wa Shekh Amri Abeid jijini Arusha leo ambapo makamo wa Rais Samia Suluhu anaongoza waombolezaji leo.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *