Watu kadhaa wamefariki baada ya moto mkubwa kuteketeza jengo refu usiku wa kuamkia leo mjini London nchini Uingereza.

Wazima moto bado wanakabiliana na moto huo katika jumba la Grenfell Tower, ambapo walioshudia walisema kuwa watu walikwama ndani, wakiitisha msaada.

Moto huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza kuwaka kuanzia mida ya saa saba usiki kwa saa za Uingereza.

Idara ya wazima moto jijini London ilituma malori 40 ya kuzima moto huo lakini jitihada zikashindikana kutokana na moto huo kuwa mkubwa.

Jengo hilo lilikubwa na wasiwasi wa kuanguka kutokana na kuteketea kwa muda mrefu na moto huo uliodumu zaidi ya masaa manne.

Zaidi ya wakati 600 jengoni humo walijaribu kujiokoa ambapo huduma za magari ya wagonjwa zimesema watu 50 wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali za jiji hilo.

Habari zaidi zinasema watu walionasa ndani yake walifunga mashuka yao na kuyatumia kama kamba na kujirusha kupitia madirishani ili kujiokoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *