Watu saba wameuawa baada ya kufyatuliwa risasi na mtu mwenye silaha kwenye nyumba moja mjini Dallas, Texas nchini Marekani.

Msemaji wa polisi David Tilley alisema kuwa mshambuliaji aliuawa na polisi kwa kwanza ambaye alifika wakatin wa ufyatulianaji wa risasi.

Kile kilichochangia shambulizi hilo bado hakijulikani au ikiwa mshambuliaji aliwafahamu waathiriwa.

Gazeti moja huko Dallas liliripoti kuwa wale waliouawa walikuwa wakitazama timu ya Dallas Cowboys, ambayo ni timu ya kandanda ya Marekani wakati walishambuliwa.

Polisi hawajatoa jina la mshambuliaji au muathirwa yeyote lakini wote wametajwa kuwa watu wazima.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *