Watu 99 wamefariki dunia na wengine wamejeruhiwa kutokana na ajali ya treni iliyotokea mapema leo kaskazini mwa India.

Treni hiyo ilikuwa ikitoka Indore kuelekea Patna kabla ya kupoteza muelekeo na kutoka katika barabara ya reli na kuanguka ilipokaribia mji wa Mashariki wa Kanpur katika jimbo la Utter Pradesh.

Maafisa wa kutoa huduma za dharura wanajaribu kuwaokoa manusura waliokwama katika mabehewa yaliyoanguka.

Waziri wa uchukuzi wa India ameamuru kufanywa kwa uchunguzi kubaini kilichosababisha ajali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *