Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limewakamata watuhumiwa 80 wanaojihusisha na mtandao wa dawa za kulevya mkoani humo.

Katika watuhumiwa hao yupo  askari Polisi mmoja mwenye namba 6978 Koplo zakayo, ambaye anashikiliwa kwa mahojiano.

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo amesema askari huyo amekamatwa kwa sababu ya kubambikizia watu bangi na kuanza kuwatisha ili apate rushwa, kitendo ambaho kinyume cha sharia.

Mkumbo amesema katika msako wa madawa ya kulevya hakuna mtu atakayebaki salama hata kama ni askari, hivyo vema watu wakaacha kujihusisha na upatikanaji wa fedha kwa njia haramu ya madawa ya kulevya.

Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa ndani ya mwezi huu walipoanza msako wa madawa ya kulevya katika maeneo mbalimbali ya Wilaya zake na Mkoa wa Arusha, ambapo walifanikiwa kukamata misokoto 3,845 ya bangi, iliyopatikana kwa watuhumiwa 54 waliokamatwa na kufunguliwa kesi katika vituo vya Polisi mbalimbali.

Aidha ametaja watuhumiwa 12 walikamatwa na Mirungi kilo 33 na watuhumiwa wengine 14 walikamatwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin kete 167.

Amesema watuhumiwa wa bangi kati yao kuna wauzaji 40, msafirishaji mmoja na wanaojihusisha na biashara hiyo 14 akiwemo askari huyo na watuhumiwa wa Heroin na mirungi walipatikana na madawa hayo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *