Watu 500 wa familia moja nchini China wamepiga picha ya familia wakiwa wote pamoja na kuleta gumzo n mitandaoni.

Picha hizo zilichukuliwa wakati wa kusherehekea mwaka mpya nchini humo ambao huadhimishwa na familia kubwa na vyakula.

Mpiga picha Zhang Liangzong alipiga picha hizo kwa kutumia ndege isiokuwa na rubani karibu na eneo la kitalii la Shishe.

Famila hiyo ikijiandaa kupiga picha.
Famila hiyo ikijiandaa kupiga picha.

Zhang Liangzong amesema kwamba familia ya Ren ambayo inatoka kijijini inadaiwa kuanza miaka 851 iliopita lakini rekodi ya udugu wao haijaangaziwa kwa zaidi ya miongo minane.

Wazee wa kijiji hivi majuzi walianza kuangazia rekodi za familia hiyo na kufanikiwa kupata ndugu wengine 2000 kupitia vizazi saba, alisema Bw Zhan.

Waliadhimisha mafanikio hayo kwa kuweka mkutano mkubwa na kuweza kupata zaidi ya wanachama 500 wa familia hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *