Watu 50 wameuawa wakati wa mandamano ya kumpinga rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila hapo jana mjini Kinshasa baada ya polisi kufyatua risasi.

Upinzani umevilaumu vikosi vya usalama kwa kutumia risasi dhidi ya maandamano yanayotaka kutangwazwe tarehe ya uchaguzi wa urais.

Upinzani umeitisha maandamano zaidi leo Jumanne ili kupinga .

Serikali ya DRC iliwalaumu waandamanaji waliokuwa wamejihami na kusema waliouawa ni watu 17 wakiwemo polisi watatu.

Waziri wa mambo ya ndani Evariste Boshab amesema mmoja wa maafisa hao wa polisi aliuawa kwa kuchomwa moto akiwa bado yupo hai.

Kuna wasiwasi kuwa rais Joseph Kabila ana njama ya kutaka kusalia madarakani baada ya kumalizika kwa muhula wake mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa katiba, muhula wa pili wa Rais Kabila, aliyeingia madarakani baada ya kuuawa kwa babake Laurent Kabila mwaka 2001, unafaa kumalizika tarehe 20 Desemba.

Tangu kujinyakulia uhuru zaidi ya miaka 55, hakuna kiongozi aliyewahi kumkabidhi mrithi wake madaraka kwa njia ya amani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *