Zaidi ya watu 39 wameuwa na wengine 25 kbaada ya moto mkubwa wa msituni kuwaka nchini humo.

Wengi wao walifariki pale walipokuwa wakiukimbia mji wa Pedrogao Grande, kilomita 50 kama (Maili 30) Kusini mashariki mwa Coimbra, kwa kutumia magari yao.

Waziri wa maswala ya ndani wa nchi hiyo João Gomes, amewaambia waandishi habari kuwa, waathiriwa 16 wameteketea ndani ya magari yao hadi kufa, pale walipokabiliwa na moto huo mkubwa katika Wilaya ya Pedrógão Grande barabara inayounganisha miji ya Figueiro dos Vinhos na Castanheira de Pera.

Kutokana na moto huo nchi ya Uhispania imetuma ndege mbili ya kuzima moto, ili kuweza kukabiliana na janga hilo.

Haijabainika kilichosababisha moto huo wa msituni, ambao umeteketeza nyumba nyingi katika maeneo hayo.

Awali, meya wa eneo hilo Valdemar Alves, aliwaambia wanahabari kuwa, kuna idadi ndogo ya wazima moto, kukabiliana na janga hilo la moto katika vijiji kadhaa ambavyo vinaungua kwa sasa.na na janga hilo la moto katika vijiji kadhaa ambavyo vinaungua kwa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *