Zaidi ya watu 36 wameuawa katika kituo cha kuchezea kamari mjini Manila nchini Ufilipino baada ya mtu mwenye silaha kuanza kuwafyatulia risasi watu waliokuwemo humo.

Wengi wa waliofariki inaaminika wamefariki kutokana na kukosa hewa safi kutokana na moshi uliotanda mtu huyo alipowasha moto meza za chumba hicho cha kamari.

Mtu huyo alianza kwa kupiga risasi skrini za TV katika chumba hicho cha Resorts World Manila leo.

Kisa hicho kimesababisha kuanzishwa kwa operesheni kali ya kiusalama nchini humo kutokana na kitendo hicho.

Maafisa awali walisema hakuna aliyekwua ameumia kutokana na kisa hicho, lakini sasa inabainika kwamba wamepataa miili ya watu wakikagua chumba hicho.

Polisi wamesema kisa hicho kinaonekana kuwa kisa cha kawaida tu cha wizi, na kwamba hakikuhusiana na ugaidi.

Polisi hao wamesema kuwa taarifa zinaonesha mtu huyo alikuwa na matatizo ya kiakili na ndiyo mana akafanya tuko hilo la kinyama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *