Jumla ya watu 36 wameuawa na weingine wamejeruhiwa nchini Misri kufuatia milipuko iliyolenga waumini wa kanisa la Coptic leo.

Watu 25 walikuwa wameuawa mapema katika kanisa la St George’s Coptic, mji wa Tanta umbali wa takriban kilomita 130 kusini mashariki.

Msaidizi wa Pope wake alisema kuwa shambulizi la Alexandria liliendeshwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga nje ya kanisa.

Kundi la Islamic State linasema kuwa ndilo liliendesha mashambulizi hayo.

Mwezi Disemba mwaka uliopita, watu 25 waliuawa wakati bomu lilipolipuka katika kanisa la Coptic cathedral mjini Cairo wakati wa sala.

Haki miliki ya picha Reuters Image caption Takriban watu 13 wameuwa kwenye mlipuko uliotokea katika kanisa moja kaskazni mwa Misri.

Ghasia dhidi ya wakiristo wa Coptic, zimekuwa nyingi miaka ya hivi karibuni, hasa tangu mwaka 2013 wakati jeshi lilipompindua rais aliyekuwa amechaguliwa.

Baadhi ya wafuasi wa rais aliyetimuliwa Mohammed Morsi, ambaye alitoka kundi la Muslim Brotherhood, waliwalaumu wakiristo kwa kuunga mkono kupinduliwa kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *