Zaidi ya watu 34 wamefariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wakati wa maandamano ya kumpinga rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila.

Maandamano hayo yanakuja kufuatia rais Kabila kukataa kuondoka madarakani licha ya uongozi wake kumalizika siku ya jumatatu.

Mazungumzo yanayoendeshwa na kanisa katoliki yanaendelea mjini Kinshasa ,ili kujaribu kumaliza mgogoro katika ya upinzani na rais Joseph Kabila ambaye amegoma kutoka madarakani.

Maafisa wa polisi wanadaiwa kukabiliana na wanachama wa kundi moja la madhehebu linaloamini kwamba mwisho wa utawala wa Kabila ndio mwanzo wa mwisho wa dunia.

Wakati huohuo Mamlaka nchini Congo imewakamata watu kadhaa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Lubumbashi.

Meya wa mji huo amesema kwamba wanajeshi walikuwa wakiwakamata wahalifu japo wenyeji wa mji huo wanasema waliokamatwa ni vijana wanaoshukiwa kupinga utawala wa rais Joseph Kabila.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *