Jumla ya watu 30 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya ajali mbaya ya lori la mizigo lililotekea kwa moto nchini Kenya.

Kwa mjibu wa naibu kamanda mkuu wa jimbo la Nakuru Isaaca Masinde, ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili katika eneo la Karai kwenye barabara ya kutoka Nairobi kuelekea Naivasha.

Lori moja lilianguka na kulipuka katika eneo la barabara hiyo yenye shughuli nyingi nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu 30 papo hapo.

Waziri wa masuala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaissery amesema kuwa watu 33 waliaga dunia wakimemo polisi 11 wa kikosi cha Recce ambacho humlinda rais na watu wengine mashuhuri.

Nkaisssery pia amesema kuwa sio gari la kusafirisha mafuta lililolipuka bali gari aina ya Canter lililokuwa na mitungi ya gesi inayoshika moto kwa haraka, iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Mombasa kwenda Kampala, Uganda,.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *