Watu 30 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama katika ziwa Albert magharibi nchini Uganda.

Abiria wengi walikuwa wanasoka na mashabiki wao waliokuwa wakielekea katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha siku ya Krismasi.

Mafisa wa polisi wamesema chombo hicho kilikuwa kimejaa kupitia kiasi huku abiria wakiimba na kupiga tarumbeta.

Boti hiyo inadaiwa kuzama katika maji yaliotulia .

Ajali hutokea mara kwa mara katika ziwa Albert ,ambapo maboti hujaa kupitia kiasi licha ya kutofanyiwa ukarabati wowote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *