Watu zaidi 250 wamefariki dunia na 400 wamejeruhiwa baada ya kufukiwa na maporomoko ya ardhi nchini Colombia.

Hata hivyo idadi hiyo huenda ikaongezeka kwani bado kuna zaidi ya watu 200 ambao hawajapatikana .

Vikosi vya wafanyakazi wanaoendesha shughuli za uokoaji wamesema nyingi ya barabara za kulipotekea maporomoko hayo huko eneo la mji wa kusini mwa taifa hilo, Mocoa hazipitiki kutokana na mkasa huo.

Viongozi wa mataifa jirani wa Mexico na Argentina walikuwa wa kwanza kutoa ujumbe wa pole na kuahidi kwenda kuisaidia Colombia.

Rais Juan Manuel Santosa alitangaza hali ya tahadhari eneo hilo na kusafiri kuangalia shughuli za uokoaji.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *