Watu zaidi ya 23 wameuawa na wengine 25 kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kufyatulia risasi waumini wa kanisa la Coptic nchini Misri.
Waumini hao waliokuwa wakisafiri kwa kutumia basi katikati mwa Misri kulingana na taarifa nchini humo.
Shambulio hilo limetokea katika mkoa wa Minya, takriban kilomita 250 (maili 155) kusini mwa Cairo, basi hilo lilipokuwa linawasafirisha kwenda kanisani.
Kumetokea visa kadha vya waumini wa kanisa la Coptic kushambuliwa, mashambulio ambayo kundi la Islamic State limedai kuhusika.
Mashambulio mawili ya mabomu ya kujitoa mhanga katika makanisa Tanta na Alexandria mnamo 9 Aprili yalisababisha vifo vya watu 46.