Zaidi ya watu 20 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya mti mkubwa kuwaangukia wakiogelea katika maporomoko ya maji eneo la Kintampo nchini Ghana.

Watu hao walikuwa wakiogelea pale upepo mkubwa ulipoangusha mti na kusababisha mkasa huo, maafisa wa huduma za dharura wamesema.

Msemaji wa taifa wa huduma za dharura Prince Billy Anaglate amesema kisa hicho kilitokea katika maporomoko ya Kintampo, katika jimbo la Brong-Ahafo.

Kikosi cha pamoja na polisi na wahudumu za dharura kilifika eneo la mkasa kuwaokoa waliokwama chini ya mti huo.

Bw Anaglate aliambia AFP kwamba wanafunzi 18 walifariki papo hapo na wengine wawili wakafariki wakitibiwa hospitalini.

ALisema watu 11 kwa sasa wanapokea matibabu, akiwemo mmoja wa maafisa wa shule hiyo aliyekuwa anasimamia ziara hiyo ya wanafunzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *