Mwanamke mmoja nchini Nigeria ameripotiwa kujitoa mhanga kwa kujilipua msikitini kaskazini mwa nchi hiyo.

Ripoti zinaonyesha kuwa watu nane wamefariki huku 18 wakiwa wamejeruhiwa vibaya baada ya mlipuko huo kutokea wakati mwanamke huyo akilazimisha kuingia katika msikiti huo.

Jenerali wa polisi mjini humo amesema kuwa mwanamke huyo amesababisha vifo vya watu wanane mjini Maiduguri.

Hapo awali mlipuko mwingine ulitokea Molai amabapo aliyejitoa mhanaga ndiye aliyepoteza maisha peke yake.

Hata hivyo mpaka sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililotangaza kufanya mashambulizi hayo.Bokoharamu wamekuwa wakifanya mashambulizi kama hayo siku za nyuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *