Jumla ya watu 18 wamefariki dunia nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kutokana na ugonjwa wa Ebola.

Hayo yamebainishwa na shirika la Afya Dunia (WHO) nchini humo baada ya kubaini kutokea kwa vifo hivyo kutokana na ugonjwa huo.

Waliokufa ni pamoja na mwanamume wa umri wa miaka 39 aliyetajwa kuwa mgonjwa sufuri na watu wawili ambao walikuwa wamekaribiana naye, WHO ilisema.

WHO iliongeza kuwa takwimu zake zinaonyesha kuwa kuna hatari kubwa eneo hilo na ndogo katika maeneo ya kimataifa

WHO ilitangaza mlipuko wa ugonjwa huo nchini DRC wiki iliyopita ambapo umekuwa tishio kwasasa nchini humo.

Zaidi ya watu 11,000 walifariki kutokana na ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika mwaka 2014 na 2015 hasa nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *