Zaidi ya Watu 17 wamefariki na wengine 60 kujeruhiwa vibaya baada ya mkanyagano kutokea kwenye uwanja wa mpira wakati wa mechi ya ligi nchini Angola.

Tukio hilo limetokea katika mji wa kazkazini mwa nchi hiyo Uige na taarifa zake kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiandamana na picha za mkanyagano huyo.

Mechi iliochezwa ilikuwa baina ya timu za Santa Rita de Cassia na Recreativo do Libolo za nchini humo.

Inadaiwa kitendo cha kundi la mamia ya watu la kuingia kwa nguvu kwenye uwanja huo ndio kilichosababisha mkasa huo.

Msemaji wa hospitali ambako waliojeruhiwa wanatibiwa amesema vifo vya wengi vilisababishwa na kukanyagwa huku wakikosa hewa ya kupumia.

Daktari mmoja amesema kuwa watu kadhaa walikosa hewa huku wengine wakiwakanyaga wengine ili kujinusuru.

Mechi hiyo ilikuwa mechi ya kwanza ya msimu katika ligi ya soka nchini humo ambayo imesababisha tukio hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *