Watu 16 wamefariki kwenye ajali ya ndege ya jeshi kwenye jimbo la Mississipi nchini Marekani.

Ajali hiyo ilitokea katika kaunti ya LeFlore karibu kilomita 160 kusini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Jackson.

Watu wote 16 waliokuwa ndani ya ndege hiyo waliangamia kutokana na ndege hiyo kuungua moto baada ya ajali hiyo.

Hakuna taarifa rasmi zilizotolewa kuhusu kilichosababisha kutokea ajali hiyo lakini uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Kwa mujibu wa jarida la jimbo la Mississipi ni kuwa ndege hiyo ilianguka katika shamba moja na mabaki yake yakatabakaa mbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *