Watu 14 wamefukiwa na udongo baada ya mgodi mmoja kuporomoka katika mkoa wa Geita walipokuwa wakiendelea na uchimbaji wa madini.

Tukio hilo limetokea saa 9 usiku jana wakati wachimbaji hao wakiendelea na shughuli ya uchimbaji katika mgodi wa RZ unaomilikiwa na wachina.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga ametembelea eneo la tukio na kuona shughuli za uokozi zikiendelea na kuagiza nguvu ziongezwe.

Kamisha msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Mhandisi Yahaya Samamba amesema jitihada zilizofanyika ni kuwasiliana na migodi iliyopo karibu na eneo hilo pia wameomba msaada kutoka Kahama na kwenye mgodi wa GGM kupatiwa vifaa vya uokoaji ili zoezi hilo liweze kufanikiwa.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita Elisa Mugisha amesema eneo la chini ambalo limefukiwa na udongo ndiyo ambalo sasa wanaendelea kulitanua ili sehemu hiyo iwe kubwa watu waweze kupita.

Mwanasheria na msemaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu ya RZ Frances Kiganga ameelezea kuwa chanzo kikubwa ni mashimo ya zamani kwani udongo unapotikisika umekuwa ukisababisha baadhi ya nyufa kuendelea kupata shida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *