Watu 12 wamefariki na wengine tisa kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya New Force kupinduka katika eneo la Ilongwe kata ya Kifanya, Mkoani Njombe na kupelekea vifo hivyo pamoja na majeruhi.

Basi hilo linalofanya safari zake kati Mkoa waNjombe na Dar es Salaam lilipinduka majira ya saa moja na dakika 40 usiku wakati likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe.

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na shirika la habari la taifa kutoka mkoani Njombe zinasema kati ya watu hao 12 wanawake ni nane akiwemo mtoto mmoja wa kike pamoja na wanaume wanne akiwemo mtoto mmoja wa kiume.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo amesema kabla ya ajali kutokea tayari basi hilo lilikuwa limeyumba karibu mara tatu na baadaye kupinduka kabisa.

Katika tukio lingine la ajali iliyotokea mkoani Kilimanjaro katika msafara wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki imesababisha majeruhi wawili akiwemo afisa wa polisi pamoja na mwandishi wa habari wa shirika la habari la taifa ambao wote wamelazwa kwa ajili ya matibabu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *