Watu 13 wamepoteza maisha na wengine 11 kujeruhiwa kwenye ajali ya basi la Super Shem lililogongana na daladala linalofanya safari zake Nyegezi na Shilima kwenye eneo la Hungumalwa mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea ajali hiyo ambayo imehusisha gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T368 CWQ na basi la Super Shem aina ya Scania lenye namba za usajili T874 CWE.

Abiria wanaodaiwa kupoteza maisha na kujeruhiwa zaidi ni wale waliokuwa kwenye daladala.

Miongoni kwa watu waliopoteza maisha ni watoto wadogo wawili.

Hii inakua ajali kubwa ya pili inayohusisha basi la abiria kutokea ndani ya wiki hii ukiacha ile iliyotokea mkoani Njombe na kuua watu 12 siku mbili zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *