Inasadikiwa kuwa takribani watu 100 wamekufa mwishoni mwa wiki kwenye mapigano baina ya polisi na waandamanaji yaliyotokea kwenye miji mbalimbali nchini Ethipia.

Kwa mujibu wa shirika la Amnesty International matukio ya mauaji yametokea kwenye mji wa Bahir Dar ambapo watu 30 waliuawa siku ya Jumapili.

Hata hivyo mamlaka za Ethiopia zimetangaza kuwa watu waliouawa ni 7 na kuwa vikosi vya usalama vilikuwa vinadhibiti fujo zilizoanzishwa na waandamanaji.

Amnesty International pia limeripoti kuwa watu 67 waliuawa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa wa Oromo ambapo polisi walifyatua risasi za moto kwa waandamanaji.

Kwenye miezi ya karibuni nchi ya Ethiopia imekumbwa na maandamano ya mara kwa mara huku watu wa mkoa wa Oromo na Amhara wakilalamika kutengwa kiuchumi na kisiasa.

Miili mingi ya watu waliouawa kwenye mapigano hayo imeendela kuzikwa tangu siku ya Jumapili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *