Watu 10 wameuawa Jumapili usiku wakati wa makabiliano kati ya wanajeshi na waasi, wanaoaminiwa kutoka nchini Uganda eneo lililo mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Raia 8 waliuawa kwa kupigwa risasi akiwemo mwanajeshi mmoja na mtu mwingine anayekisiwa kuwa muasi.

Wanamgambo wa ADF kutoka nchini Uganda wanaoipinga serikali ya rais Yoweri Museveni wamekuwa wakiendesha harakati eneo hilo kwa miongo miwili.

Serikali na Umoja wa Mataifa wamewalaumu ADF kwa misururu ya mashambulizi eneo hilo.

Takriban raia 700 wameuawa kwa muda wa miaka miwili iliyopita kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu linalosema kuwa haijulikani ni nani amehusika na mauaji hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *