Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kupitia kikosi cha kupambana na uhalifu wa kutumia silaha za ujambazi limefanikiwa kuwakamata wanawake wanne na watoto wanne waliokuwa wamefichwa kwenye kambi wakifundishwa mbinu za uhalifu.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kupatikana kwa wanawake na watoto hao ni baada ya mzazi mmoja aliyejulikana kwa jina la Shaban Abdalla mkazi wa kitunda jijini Dar es salaam kutoa taarifa polisi kuwa watoto wake wanne wametoroshwa na mtalaka wake aliyejulikana kwa jina la Salma Mohamed kwahiyo jeshi hilo likafanya msako likafanikiwa kuwakamata watoto na wanawake hao huku mtoto mmoja akiwa ni wa mzazi huyo.

Kamanda Sirro amesema wakati wakihojiwa kati ya wanawake hao ambao wamekamatwa amesema baada ya kufikishwa katika eneo hilo la Vikindu mkoani Pwani walimtaka abadilishe jina lake la kikristo na aitwe jina la Kiislamu na kumtaka kukaa pale kwaajili ya kuwapikia watoto hao pasipo mama huyo kujua watoto hao wametoka wapi.

Aidha Kamanda Sirro alitoa wito kwa wazazi na walezi na walezi kuwa “Si busara kwa sisi walezi au wazazi wa hawa watoto hawa watoto bado wanahitajika ndiyo tunasema taifa la kesho watoto wapate elimu ya msingi ambayo itasaidia katika maisha yao ya kila siku,tusiwaingize kwenye elimu ambayo mwisho wa siku sana sana watapoteza maisha yao kwahiyo hao watoto tupo nao na tutahakikisha kwamba tunawarudisha kwa wazazi wao”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *