Aliyekuwa mshindi wa BSS Water Chilambo ameziomba TV na Radio kuacha kupiga nyimbo zake za bongo fleva kwa sasa na wamsapoti kwenye muziki wa Gospel ambao anaufanya.

Chilambo amesema wametokea wasanii wengi pamoja na waandaaji wa muziki kumuita ili waweze kufanya kolabo ya nyimbo ya bongo fleva lakini aliwakatalia hali iliyowapelekea wengine kutokumuamini na kuhisi kwamba anaringa.

Pia amesema kuwa ameamua mwenyewe kubadilika na kuingia kwenye nyimbo za injili na kumtumikia Mungu na hakuna shida yoyote aliyoipitia wala hajashauriwa na mtu yeyote kuingia kwenye nyimbo za injili bali alijikuta tu mwenyewe anaingia kwenye muziki wa injili na kuupenda zaidi.

Siwezi kumridhisha kila mtu bali namuangalia Mungu wangu sitaweza kuingia kwenye akili za watu kuwaambia kwa sasa nafanya muziki wa injili hivyo nawasihi wasanii wenzangu pamoja na media kunisapoti huku kwenye muziki wa injili kwani nimeamua kumtumikia Mwenyezi Mungu kutoka moyoni na siyo vinginevyo”. 

Mwanamuziki huyo kwasasa ameamua kufanya muziki wa Injili kwa hiyo ameamua kuachana na muziki wa Bongo Fleva aliokuwa anaufanya hapo awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *