Watanzania 25 wamekamatwa katika nchi za China, Brazil na Zambia kutokana na makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2015 ambayo iliwasilishwa bungeni jana.

Akizungumza jana baada ya shughuli za Bunge, Mavunde amesema Watanzania hao 25 wamekamatwa na wanatumikia vifungo mbalimbali.

Mavunde amesema taarifa hiyo inaonesha kuwa mwaka jana, biashara ya dawa za kulevya iliendelea kufanyika kwa kiwango kikubwa na kasi. Dawa aina ya mandrax ya kilogramu 5.1 ilikamatwa Dodoma na Ruvuma.

Amesema mara ya mwisho dawa hiyo ilikamatwa mwaka 2010 nchini.

Amesema pia bangi bado ni tatizo na kwamba hekta 50 za bangi zilichomwa huku kilogramu 161 za heroin zikiteketezwa Dar es Salaam na Tanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *