Polisi nchini Jamhuri ya Dominica inawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya watangazaji wawili waliouawa wakati wakiendesha kipindi cha redio.

Kwenye mkasa huo, mwandishi mmoja wa habari alikuwa akirekodi kipindi chake LIVE kwenye mtandao wa Facebook kabla ya kupigwa risasi na kuuawa.

Kipande cha video kinachoonyesha tukio hilo, kimeonyesha matangazo hayo ya moja kwa moja yakivurugwa na sauti ya mwanamke anayesikika akipiga kelele za ‘risasi, risasi, risasi’

Maafisa usalama wamedai kuwa mauaji hayo yametokea siku ya jana kwenye mji wa San Pedro de Macoris, mashariki mwa mji mkuu wa Santo Domingo.

Watangazaji waliouawa kwenye tukio hilo ni Luis Manuel Medina na prodyuza wa redio hiyo, Leo Martinez.

Mwanamke aliyesikika akipiga kelele naye pia amejeruhiwa na polisi wamesema amekimbizwa hopspitali kwaajili ya kufanyiwa upasuaji.

Hata hivyo watuhumiwa hao bado hawajafunguliwa mashtaka kwa kile polisi ilichodai hawajua chanzo cha mauaji hayo.

‘Uchunguzi umeanza na tutajitahidi kwa kutumia uwezo wote tulionao kuufikia ukweli’. Amesema Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo, Jean Rodriguez

Mauaji kama hayo yaliwahi kufanyika nchini Marekani mwaka 2015 wakati waandishi wawili walipouawa wakati wakifanya matangazo ya moja kwa moja kwenye jimbo la Virginia.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *