Juhudi za uokoaji za kuwanasua watalii 45 ambao wamekwama kwenye magari ya kutumia kamba katika mlima wa Mont Blanc nchini Ufaransa zimeanza tena.

Watalii hao walilala usiku wa Alhamisi kwenye kibaridi kikali wakiwa wamekwama juu ya barafu takriban 3,800m (futi 12,468) juu mlimani.

Walikuwa miongoni mwa watu 110 waliokwama baada ya magari hayo kupatwa na hitilafu Alhamisi alasiri.

Inaaminika magari hayo yalikwama baada ya kamba kushikana kutokana na upepo mkali.

Watu 65 waliokolwa kwa kutuia helikopta baadaye Alhamisi lakini juhudi zikasitishwa giza lilipoingia na kukawa na mawingu hivyo kuifanya vigumu kuona.

Mkuu wa idara ya uokoaji ya Haute-Savoie, Georges Francois Leclerc  amesema kuwa walilazimika kusitisha juhudi za uokoaji kwa sababu za kiusalama ambapo sasa wameendelea na zoezi hilo.

Pia msemaji huyo amesema kwamba wanatumai watawapata wote salama ambapo juhudi za uokoaji zinaendelea nchini Ufaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *