Muigizaji nyota wa Bongo movie, Wastara Juma amekuwa balozi wa Kampuni ya simu ya mkononi ya KZG ambapo leo amekabidhiwa na kusainishwa mkataba rasmi.

Akizungumza katika tukio la kusaini makubaliano ya kuwa balozi wa kampuni hiyo  lililofanyika katika ukumbi wa De Mag Hotel iliyopo Mwananyamala, Dar,  Wastara amesema amefurahi sana kupata shavu hilo kwani kujituma kwake katika biashara ndiko kulikompatia bahati hiyo.

Amendelea kusema kwamba atahakikisha anafanya vizuri katika ubalozi huo ambao kwa mwaka unampatia shilingi milioni mia nne kutegemea na jinsi kampuni hiyo inavyouza bidhaa zake hizo kwani imempa heshima kubwa ambayo hakuitarajia.

Katika tukio hilo pia kampuni hiyo ilimzawadia keki Wastara ikiwa ni zawadi ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kwani ilikuwa jana, hivyo kutokana na nafasi hiyo wakaona ni vyema wampe zawadi hiyo iliyokuwa imechorwa aina mojawapo ya simu za KZG.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *