Muigizaji nyota wa Bongo movie, Wastara Juma ameamua kurudiana na mpenzi wake Bond Bin Sinan baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake, Sadifa Khamis Juma.

Wastara amesema Bond Bin Sinan amekiri makosa yake kwenye vyombo vya habari ndio maana imekuwa rahisi kwake kumsamehe na kurudiana naye.

Muigizaji huyo amesema “Makosa yake aliyokuwa ameyafanya mwanzo ndiyo yaliyosababisha tukaachana nikaamua kuolewa na mtu mwingine.

Wastara na Bond: Wakiwa katika pozi la mahaba
Wastara na Bond: Wakiwa katika pozi la mahaba

Pia aliongeza kwa kusema “Kwa hiyo baada ya mimi kuachana na aliyekuwa mume wangu na yeye bado alikuwa ananihitaji, nikaona nimkubalie kwa sababu tayari tulikuwa tunafahamiana naye,”.

Bond na Wastara walikuwa wapenzi kabla ya kuachana na Wastara kuamua kuolewa na Sadifa Khamis Juma ambaye ni mbunge wa Donge pia ni mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM Taifa ambao pia wameachana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *