Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imewakamata wasichana 13 kutoka nchi za Nebal na India wenye umri kati ya miaka 18 na 26 ambao wameletwa nchini kinyume cha sheria na kuendesha biashara ya ukahaba.

Kamishna wa Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam, John Msumule amesema mbali na raia hao wa kigeni pia wamewakata raia wa Kitanzania mbao wanashirikiana na wahamiaji hao.

 

Amemtaja Mohamed Shabani Magamba ambaye anatengeneza vibali vya kugushi ambapo pia amekutwa na pastpoti za 4 za raia wa nchi za Nigeria, Botswana, Somalia na Uingereza.

 

Pia Msumule ameitaja Wilaya ya Kinondoni kuwa inaongoza kwa kuwa na Madanguro ikifuatiwa na Temeke ambapo kwa sasa wanajipanga kuyaondoa kwa muda wa siku 10 madanguro hayo pamoja na kuendesha oparesheni kubwa katika Mitaa ya Msimbazi, Lumumba na Uhuru katika soko la Kariakoo hna maeneo ya Mtoni Mtongani na Sabasaba ambako wamekwisha yafanyia uchunguzi wa kina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *