Maafisa wanne wa polisi katika kituo cha Syokimau nchini Kenya wamefikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji ya watu watatu ambapo wakili na mteja wake pamoja na dereva wa taksi waliuawa.

Maafisa hao Fredrick Leliman,na Leonard Maina Mwangi, pamoja na koplo wa polisi Stephen Chebulet na konstebo Silvia Wanjiku Wanjohi wamefikishwa mbele ya Hakimu mkuu wa Mlimani, Jaji Jessy Lesit ambapo kila mmoja alisomewa mashtaka matatu ambapo walikana mashtaka hayo.

Maafisa hao wanatuhumiwa kwa kosa la kuwateka nyara na kuwaua wakili Wille Kimani na mteja wake Josephat Mwenda pamoja na dereva wao wa taksi, Joseph Muiruri katika mji wa Mavoko jijini Nairobi.

Washtakiwa wote wamerudishwa rumande na kesi hiyo itasikilizwa tena Agosti 16 mwaka huu.

Wakili Kimani: Enzi za uhai wakeWakili Kimani: Enzi za uhai wake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *