Wafanyakazi kusini mwa India wamepewa likizo kutokana na uzinduzi wa filamu ya muigizaji, Rajinikanth inayoitwa kwa jina la “Kabali” ambayo itaoneshwa katika kumbi za sinema  nchini humo.

Hatua hiyo imefikiwa mara  baada ya wafanya kazi wengi kutumia visingizio tofauti wakati wa muda wa kazi ili waingie kwenye kumbi za sinema.

Rajinikanth, ni mmoja wa waigizaji wanaolipwa pesa nyingi sana katika bara la Asia na mmoja wa waigizaji mashuhuri zaidi kutoka nchini India.

Filamu hiyo ya “Kabali” itaonyeshwa katika kumbi 12,000 za sinema nchini India kuanzia leo, ambapo kabla ya kuzinduliwa imejizolea $30m (£20m) kupitia mauzo ya haki zake.

Kabali ni filamu ambayo inaangazia uhalifu wa magenge itatolewa pia kwa lugha za Kitelugu, Kihindi na Kimalay.

Katika miji kama vile Chennai na Bangalore, baadhi ya kampuni zimetangaza leo kuwa siku ya likizo na hata kuwapa wafanyakazi tiketi za bure wakatazame filamu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *