Raia wa Palestina wanaoishi kwenye meneo yanayotambuliwa kama maeneo ya waizraeli wamefanya maandamano hadi kwenye bunge la Israel ‘Knesset’ lililopo Jerusalem Magharibi kupinga uvunjwaji wa makazi ya wapalestina.

Maandamano hayo yaliyofanyika jana yanafuatia baada ya mamlaka ya Israel kupitisha azimio la ujenzi wa makazi ya walowezi yapatayo 566 kwenye eneo walilolivamia la Jerusalem Mashariki kitendo ambacho kimelaaniwa na viongozi wa mamlaka ya Palestina.

Makazi hayo ya kilowezi yapo kinyume cha sheria ya kimataifa.

Israel imekuwa ikiikalia kwa mabavu ardhi ya wapalestina kwa miaka mingi na licha ya jitihada za Umoja wa Mataifa za kumaliza mgogoro lakini kinyume chake ni kuwa Israel inazidi kujitanua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *