Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa amewataka wananchi kwa ujumla wanaofanyiwa vitendo vya uhalifu mitandaoni wasiende TCRA bali wanapaswa kutoa taarifa katika jeshi la polisi.

ACP Mwakalukwa amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza katika mkutano wa pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu suala zima la uhalifu wa makosa ya mitandao ambapo kwa sasa limeshika kasi kubwa

Pamoja na hayo, ACP Mwakalukwa ameendelea kwa kusema “Kutokana na kukua kwa teknolojia vitu vingi vimekuwa vikifanyika ‘online’ kwa hiyo hii mitandao ya kijamii imeonekana ni muhimu sana kwenye maendeleo.

Pia amesema kuwa mitandao hiyo imebadilisha mbinu ya kufanya uhalifu katika mitandao ya kijamii kwa kutumiwa na baadhi ya watu kutapeli, hata kutishia kuua, hivyo jeshi la polisi limejipanga kwa ajili ya kushughulikia makosa ambayo yanatokana na mtandao.

Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa TCRA, Thadayo Ringo amesema analishukuru jeshi la polisi kwa kuweza kuwasaidia katika kuwatatulia changamoto mbalimbali hasa za kiusalama huku akiwataka wananchi watakaopata matatizo katika mtandao kwenda kutoa taarifa polisi ili waweze kuwasaidia kabla ya kufika kwao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *