Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli toka atangaze uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma, kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini kutaka viwanja mkoani humo.

Hadi sasa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) imepokea maombi 3,500 ya watu wanaotaka viwanja vya kujenga majengo mkoani humo.

Wafanyabiashara katika masoko mbalimbali ya Dodoma wamesema hawana mpango wa kupandisha bei ya vyakula hata serikali itakapohamia rasmi, kwani vipo vingi na wamejipanga kuongeza mitaji ili kuendana na kasi ya ongezeko la watu.

Dodoma: Baadhi ya maeneo ya mji mkuu Dodoma ambapo Serikali itahamia.
Dodoma: Baadhi ya maeneo ya mji mkuu Dodoma ambapo Serikali itahamia.

Ofisa Uhusiano wa CDA, Angela Msimbira amesema mpaka sasa maombi yaliyopokelewa ni takribani 3,500 kwa ajili ya viwanja vya makazi na taasisi mbalimbali.

Pia amesema wizara karibu zote zimeshatuma maombi ya kupatiwa maeneo, mifuko ya hifadhi ya jamii, makanisa, shule, vyuo, Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na watu binafsi kwa ajili ya kupata maeneo mkoani humo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *