Wananchi wa Jimbo la Igunga Mkoani Tabora wamemtaka Mbunge wao Dk. Dalaly Kafumu ajiuzulu ubunge kwa walichodai ni kushindwa kutumia madaraka yake vizuri wakati akiwa Kamishna wa Madini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti , baadhi ya wananchi hao, Oscar Thomas, Godfrey Batoba, Pius Roben na Regina Jackson, walisema ni vema mbunge wao akajiuzulu kwa kuwa miongoni mwa wanaotuhumiwa kuiingizia hasara nchi kwa kuingia mikataba mibovu ya madini na kujinufaisha.

Thomas alibainisha kuwa kazi anayofanya Rais John Magufuli ya kufuatilia rasilimali za wananchi inapaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania mwenye uchungu na nchi yake huku wakimwomba kutoonea huruma wahusika walioisababishia nchi hasara.

Mwenyekiti wa Wazee wa Wilaya, Kassim Ally akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake, alisema walimwomba Rais Magufuli kutokatishwa tamaa na baadhi ya viongozi wasio waaminifu kwani wako nyuma yake wakimpa ushirikiano.

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya, Costa Ollomi na wakem, Mwanamvua Killo walisema kazi anayofanya Rais Magufuli imeleta heshima ndani ya chama na Serikali na kuwataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati waliohusika wakihojiwa na vyombo husika.

Kuhusu Mbunge kujiuzulu alisema Ollomi alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa tayari Rais alishatoa maelekezo ya kuchukuliwa hatua kwa waliotajwa na Kamati.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *