Zoezi la Upimaji wa Afya Bure kwa muda wa siku tano limeanza leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Wananchi wa jiji la Dar es Salaam wameanza kuwasikli katika viwanja hivyo vya mnazi mmoja kuanzia saa 10 usiku.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza zoezi la Upimaji bila Malipo kwa wakazi wa Dar es Salaam kwa ajili kujua afya zao.

Madaktari bingwa na Wauguzi kutoka Hospital za Umma, Jeshi na zile za Watu Binafsi wanaendelea na zoezi la Upimaji kwa Wananchi.

Katika Upimaji huo Mwananchi atakaepimwa na kubainika kuwa na matatizo ya kiafya atapelekwa Hospital na kupatiwa Matibabu Bure.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *