Raia nchini Angola leo wanapiga kura kumchagua rais mpya wa nchi hiyo baada ya miaka 38 ya Rais Jose Eduardo dos Santos.

Rais Jose Eduardo dos Santos amekuwa madarakani tangu mwaka 1979 na kuwa rais wa pili barani Afrika kuwa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi.

Rais Santos hawanii tena uchaguzi huu, ambao waziri wa ulinzi Joao Lourenco anawania kama mgombea kupitia chama tawala cha MPLA.

Mpinzani wake mkuu anatarajiwa kuwa Isias Samakuva, kutoka chama cha hasimu wa MPLA, Unita.

Wachangazi wanasema kuwa chama cha MPLA ambacho kimekuwa madarakani tangua uhuru wa nchi hiyo mwaka 1975, kinaokana kuwa kitaibuka mshindi.

Chama cha tatu kwa ukubwa cha Casa-CE, kinaongozwa na Abel Chivukuvuku, ambaye alikuwa afisa wa cheo cha juu wa Unita wakati kilikuwa ni kundi la waasi.

Baada ya vita, Angola ilikuwa moja ya nchi zilizokuwa aa uchumi uliikua kwa haraka zaidi duniani kutona na utajiri wake mkubwa wa mafuta.

Ikiwa asimia kubwa ya watu wako chini ya umri wa maiak 35, watu hao ndio na watakuwa na uamuzi mkubwa

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *