Mwanamuziki mtata wa hip hop Bongo, Nay wa Mitego ameweataja wanamuziki watano wa hip hop anaowakuli zaidi na upenda kuwsikiliza kutokana na kazi zao.

Nay wa Mitego amesema msanii wa kwanza ambaye yeye anakumbali na kumuheshimu ni Mr 2 (Sugu) kwani huyo ndiye aliyemfanya yeye kuanza kuimba na anatamani kuona anaendelea kufanya muziki siku zote kwani akiwa anasikiliza kazi zake mpaka leo huwa anafurahi.

Pia wa pili anayemkubali ni Fareed Kubanda, wa tatu ni Mr Blue, wa nne ni Mwana FA na rappa watano ni Nay wa Mitego mwenyewe ambaye anajua mashabiki zake wanataka nini na kuwapa muziki mzuri siku zote.

Mkali huyo hivi karibuni ameingia kwenye headline za mashabiki baada ya kuposti maneno kwenye akaunti yake Instagram akimaanisha kuuponda wimbo wa Madee ‘Hela’ ambao ni mpya uliotoka wiki hii.

Mwanamuziki huyo ni miongoni mwa wasanii wa hip hop wanaofanya vizuri kwenye muziki wa Bongo kutokana na nyimbo zake kuwaburudisha mashabiki zake kutokana na mahudhui ndani ya nyimbo hizo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *