Wanamuziki wa dansi wa Tanzania leo wanatarajia kuungana na  kufanya tamasha ambalo litafanyika katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Tanzania Band Festival, lina malengo ya kumsapoti Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika kampeni yake ya kuchangia madawati mashuleni kwani sehemu ya mapato ya tamasha hilo yatakuwa kwa ajili ya kampeni hiyo.

Mratimbu mkuu wa tamasha hilo Sidi Mfaume amesmema kwamba wameamua kushirikiana ili kumsapoti mkuu wa mkoa Makonda kwa namna anavyojitolea katika kuwasaidia wanafunzi lakini hata yeye amekuwa akiusapoti Muziki wa Dansi.

 Katika tamasha hilo  kutakuwa na bendi kumi zitakazoshiriki ambazo ni  Msondo Ngoma,Sikinde, Mapacha wa Tatu,Yamoto Band, Banana Zorro,Tip Top,Syklight, FM Academia na nyingine nyingi huku kiingilio kikiwa shilingi 15,000 tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *