Wanajeshi wa Ivory Coast wameondoka kwenye barabara za mji wa pili kwa ukubwa, Bouake ambako walianza kuasi Ijumaa iliyopita wakitaka kuboreshwa kwa mishahara yao.

Hatua hiyo inafuatia tangazo la Rais Alassane Ouattara kwamba amefikia makubaliano kuhusu pato na marupurupu yao.

Uasi huo ulitapakaa hadi sehemu nyingine za nchi, lakini wakazi wa miji iliyoathirika wanasema maisha yamerudi katika hali ya kawaida, na kwamba barabara na maduka yamefunguliwa.

Waziri wa Ulinzi, Alain Richard Donwahi ameachiwa huru baada ya kuzuiliwa kwa saa kadhaa na wanajeshi ambao walikuwa hawajaridhika na mapendekezo ya serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *