Serikali nchini Uturuki imetoa vibali vya kukamatwa kwa wanahabari 40 kufuatia jaribio la mapinduzi lililotokea mwezi huu nchini humo.

Miongoni mwa wanahabari hao ni mchanganuzi mashuhuri nchini humo, Nazli Ilicak ambaye aliwahi kuwa mbunge wakati mmoja.

Maelfu ya watu wamekamatwa na kuzuiliwa tangu kutekelezwa kwa jaribio la kupindua serikali mapema mwezi huu.

Jana, maelfu ya watu walihudhuria mkutano wa vyama kadha vya siasa kupinga jaribio hilo la mapinduzi ya serikali ya rais Recep Tayyip Erdogan.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *