Makamo wa Rais, Samia Suluhu amesema kuwa madaktari watalii waliotoa msaada wa awali baada ya ajali iliyowaua wanafunzi na waalimu wa Lucky Vicent Academy wameahidi kuwapatia msaada majeruhi watatu waliobaki hospitalini hata kuwapeleka nje ya nchi kama itahitajika.

Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu amesema kwamba Madaktari hao walikuwa watalii na gari lao lilikuwa mbele ya basi la wanafunzi na hata baada ya ajali kutokea wao ndio walikuwa watu wa kwanza kutoa msaada wa kitaalamu.

Makamo wa Rais, Samia Suluhu akimuangalia mmoja wa wanafunzi majeruhi ambaye alinusurika kwenye ajali hiyo.
Makamo wa Rais, Samia Suluhu akimuangalia mmoja wa wanafunzi majeruhi ambaye alinusurika kwenye ajali hiyo.

Katika hotuba yake Makamu wa rais amesema kuwa hata baada ya kutoa msaada watalii hao  kutoka shirika la afya nchini Marekani wameahidi kujitolea kuwapatia matibabu wanafunzi watatu ambao ni majeruhi wa ajali hiyo na hata msaada kutoka nje ya nchi  wapo tayari kututoa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *